KESI YA ERICK KABENDERA YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 27 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 14, 2020

KESI YA ERICK KABENDERA YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 27

  Malunde       Tuesday, January 14, 2020

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo umebakia katika maeneo machache kukamilika. 


Wakili wa Serikali, Ester Martin ameileleza Mahakamani hiyo jana  Jumatatu, Januari 13, 2020 wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Janeth Mtega upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba wanamalizia vitu vichache ili kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Hakimu Mtega baada ya kueleza hayo, aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, 2020 itakapotajwa.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh173 milioni, katika Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post