JAMAA ALIYEIBA CHUPI 100 ZA WANAWAKE TOFAUTI TOFAUTI AKUTWA AMEVAA MBILIMwanaume mmoja mwenye tabia ya Wizi wa nguo za ndani za wanawake, anayejulikana kwa jina la Mukoshi Chipukosia (36), kutoka kijiji cha Hirumbi nchini Kenya, amekamatwa na kufikishwa kwa Mjumbe wa Nyumba Kumi kwa kosa la kuwaibia wanawake nguo za ndani 'chupi' 100 na kukutwa amevaa mbili.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Nyumba Kumi amesema, mwizi huyo amekutwa hadharani akiwa amevaa nguo hizo, wakati anajaribu kuiba zingine kwenye kamba na ndipo Mbwa wa ulinzi wa eneo hilo akaanza kubweka na kumshtua mmiliki.

Aidha mmoja wa wamiliki wa nguo hizo amesema, alikuwa anachunga Ng'ombe ghafla akasikia Mbwa wake anabweka na alipoenda akamkuta mwizi huyo anaiba.

"Tumechoshwa na hii tabia, anachofanya sio tabia nzuri, anaiba nguo za ndani za wanawake pekee, kwanini isiwe na za wanaume, kila mara anatuibia sisi tu inatushangaza ni aina gani ya wizi huu bora angeiba Kuku, Mbuzi au Ng'ombe ila sio nguo za ndani imetushtua sana" amesema mmoja wa waathirika wa wizi huo.

Pia mwizi huyo amejitetea kwa kusema yeye ni maskini, hana pesa za kununua nguo za ndani za kiume kwa hiyo ilikuwa inamlazimu kuiba na kuahidi kuwa hatorudia tena.

Chanzo ni Tuko News na K24 Tv.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post