COSTECH YATOA MAFUNZO YA HAKI MILIKI KWA WABUNIFU WALIOSHINDA MASHINDANO YA UBUNIFU


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia (COSTECH) Dkt.Athuman Mgumia katika akieleza waandishi wa habari lengo la mafunzo hayo
Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Bi.Judith Kadege akifafanua juu ya umuhimu wa haki miliki bunifu.
Mhandisi Kennedy Mwakatundu (wa pili kushoto),Mbunifu ambaye ametengeneza mashine ya kusafisha fukwe za bahari akizungumza.
Mbunifu wa kitanda cha kuweka kwenye gari la wagonjwa ambacho kinajiendesha chenyewe, Mhandisi Diana Kaijage (wa kwanza kulia) akizungumza.

Wabunifu nchini wametakiwa kujua jinsi ya kulinda bunifu zao ili zisiweze kuibiwa sambamba na kujua njia wanazoweza kuzitumia kwa kujua aina gani ya miliki bunifu zinazohitajika kwa bunifu zao.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya Haki Miliki kwa wabunifu 60 walioshinda kwenye mashindano ya sayansi na teknolojia na Ubunifu yaliyotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Bi.Judith Kadege alisema Wao wapo kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwashauri wadau tofauti katika sekta ya utafiti na ubunifu nchini lengo ni kukuza teknolojia zaidi na kupanua Wigo wa kufikia kimataifa zaidi.

Alisema elimu ya miliki bunifu inasaidia kujua haki za wabunifu kabla ya kuanza kubuni kitu ambacho wanakifikiria.

“Yote hayo tunafundisha ili kulinda ile miliki bunifu yake isije ikaibiwa, au ikatumiwa ndivyo sivyo bila ya idhini yake ama kibiashara au kwa matumizi mengine,” alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia katika Tume hiyo, Dkt.Athuman Mgumia alisema Mafunzo yataeasaidia wao kujua namna ya kumiliki bunifu zao pamoja na kuboresha teknolojia na kufika kwa Jamii.

Aidha Mhandisi wa Mitambo ambaye ni mbunifu aliyebuni mashine ya kusafisha Fukwe za bahari Kennedy Mwakatundu, alikiri kuwa Kama Wabunifu kuna vitu haviwalindi kisheria lakini kwa Mafunzo hayo wataweza kujua haki zao kisheria.

“Mafunzo haya yametujengea uelewa Mpana wa namna ya kujua sheria inasemaje hasa katika kulinda bunifu zetu hivyo tutaweza kuomdokana na kuibiwa kazi zetu”Alisema

Hata hivyo wabunifu hao waliomba mafunzo hayo yawe yanatolewa hata kwenye ngazi za chini kwa watoto wadogo ili wakue wakiwa wanauelewa wa namna ya kujua teknolojia zilivyo na wao wanaweza kuwa na ubunifu gani katika jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post