BAADA YA SUMAYE, KIGOGO MWINGINE CHADEMA ATANGAZA KUJIUZULU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, December 4, 2019

BAADA YA SUMAYE, KIGOGO MWINGINE CHADEMA ATANGAZA KUJIUZULU

  Malunde       Wednesday, December 4, 2019

Mratibu wa CHADEMA  Kanda ya Pwani, Casmir Mabina amewasilisha barua makao makuu ya chama hicho ya kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa kanda hiyo ambayo yamemfanya aliyekuwa mgombea uenyekiti, Fredreck Sumaye atangaze kukihama chama hicho.


Mabina ameeleza uamuzi wake huo leo Jumatano Desemba 4, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


“Haya Mambo yametokea ndani ya eneo langu la kazi na kwa maana hiyo leo Jumatano nimewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi yangu.

"Nitabaki kuwa mwanachama mwaminifu wa chama chetu na nitakuwa tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika.” Amesema


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post