WANAJESHI WA CHINA WASAFISHA MITAA YA HONG KONG ILIYOKUWA IMEFUNGWA NA WAANDAMANAJI


Wanajeshi wa China wametoka jana katika kambi zao mjini Hong Kong na kwenda mitaani kusaidia kuisafisha na kuondoa vifusi na vizuizi vilivyowachwa na waandamanaji.


Lilikuwa tukio lisilo la kawaida kwa Jeshi la China kuingia katika mitaa ya jimbo hilo lenye mamlaka ya ndani, ambalo kushindwa kwa serikali yake kumaliza maandamano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi mitano kumezusha uvumi kuwa China huenda ikawatumia wanajeshi wake kisiwani humo.

Serikali ya Hong Kong imesema haikuomba msaada wa jeshi katika shughuli ya usafishaji, ikiielezea kuwa shughuli ya kujitolea ya kijamii. Wengi wa waandamanaji wanaoipinga serikali waliondoka kwenye vyuo vikuu vya Hong Kong baada ya kuvidhibiti kwa karibu wiki moja.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527