SERIKALI YAAMUA KUMFARIJI BINTI AMBAE ALIFICHWA KUFARIKI KWA WAZAZI WAKE WOTE NA NDUGU ZAKE WATATU | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, November 17, 2019

SERIKALI YAAMUA KUMFARIJI BINTI AMBAE ALIFICHWA KUFARIKI KWA WAZAZI WAKE WOTE NA NDUGU ZAKE WATATU

  Malunde       Sunday, November 17, 2019

Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole.

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake Twitter kufuatia jana mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake wamezikwa baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji.

Waziri Ummy ameandika kuwa; "Suala la mtoto Anna Zambi, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba” – Waziri Ummy

Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post