WAGOMBEA 1,851 WA VYAMA VYA UPINZANI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MKOANI RUKWA

Wagombea wa vyama vya upinzani wapatao 1,851 kushiriki katika nafasi mbalimbali za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini tarehe 24.11.2019 ili kuwapata wawakilishi katika ngazi ya kijiji, mtaa, kitongoji pamoja na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wa viti maalum katika ngazi hizo.


Taarifa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa inasema kuwa wagombea hao hawatakuwa na uwezo wa kuweka mawakala kisheria kwasababu mawakala hao wanatakiwa kuwa na kiapo cha kisheria pamoja na utambulisho kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa ni isipokuwa mgombea mwenyewe ndiye anaweza kuwa wakala.

Aidha, ametahadharisha kuwa endao kutatokea vurugu katika maeneo ambayo kwasababu nembo ya chama cha upinzani imetumika wakati mgombea amejitoa ambapo yawezekana alijitoa kwa kuchelewa au aliamua kutosumbuka kujitoa,Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zitaimarisha ulinzi katika maeneo ya kupiga kura.

Idadi ya wagombea wa vyama vya upinzani waliobakia Mkoani Rukwa baada ya mwisho wa tarehe ya kujitoa 16.11.2019 saa 10 jioni ni katika vijiji 67 (19.7%), Vitongoji 348 (19.1)%, mitaa 9 (5.4%), wajumbe mchanganyiko 876 (11.8%) na wajumbe wa viti maalumu 551 (19.1%). Mkoa una jumla ya vijiji 339, vitongoji 1,817, mitaa165. Wajumbe mchanganyiko 7,420 na wajumbe wa viti maalum 2,875.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527