‘TIGO BUSINESS’ YACHOCHEA MAGEUZI YA KIDIGITALI KWENYE BIASHARA TANZANIA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 5, 2019

‘TIGO BUSINESS’ YACHOCHEA MAGEUZI YA KIDIGITALI KWENYE BIASHARA TANZANIA

  Malunde       Tuesday, November 5, 2019

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari akizungumza na wangu waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa huduma na bidhaa zilizoboreshwa zaidi pamoja na tovuti inayompa mteja mamlaka ya kujihudumia na kudhibiti matumizi ikiwa na lengo la kuzisaidia kampuni mbalimali kukuza huduma zao kidigitali.Hafla hiyo ilifanyika mapema Jijini Dar es salaam. 
Kandambara Maita..Mkuu wa Mauzo- Tigo business. akifafanua jambo kwa wageni waalikwa ( hawapo pichani) katika Hafla ya uzinduzi wa huduma na bidhaa zilizoboreshwa zaidi pamoja na tovuti inayompa mteja mamlaka ya kujihudumia na kudhibiti matumizi ikiwa na lengo la kuzisaidia kampuni mbalimali kukuza huduma zao kidigitali.
Dar es Salaam. Novemba 4, 2019. Kampuni ya Tigo kupitia kitengo cha Tigo Business leo imezindua huduma na bidhaa zilizoboreshwa zaidi pamoja na tovuti inayompa mteja mamlaka ya kujihudumia na kudhibiti matumizi ikiwa na lengo la kuzisaidia kampuni mbalimali kukuza huduma zao kidigitali.

Aidha tovuti hiyo itawasaiidia wateja kujua matumizi yao kwa wakati na kuwapa wateja mamlaka ya kusimamia akaunti zao.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari alisema “Tigo business ni huduma inayokua kwa kasi ikiwalenga hasa wafanyabiashara na inaongoza katika huduma zenye ubunifu kwenye soko la mawasiliano.Pia, ni washirika wa teknolojia na washauri wa kimkakati kwa biashara za aina zote.” 

Karikari alisema Tigo kama kampuni ya kidigitali ipo mstari wa mbele katika ukuzaji wa teknolojia na kuwa imejizatiti katika kuhakikisha kampuni zinafikia malengo ya kutoa huduma zao kidigitali sokoni.

“Bidhaa zetu ni pamoja na huduma za sauti, data, IoT pamoja na jumbe (Bulk SMS) zinazomruhusu mteja kuwasiliana na wateja wake kwa viwango nafuu.Tovuti hii pia inatoa intaneti mahsusi kwa kampuni ambazo zinahitaji suluhisho kubwa ili kuongeza ufanisi kwenye taasisi. Biashara ambazo zina matawi mengi zinaweza kuunganisha data, mifumo yake na uendeshaji kwa kutumia huduma ya ‘inter-branch connectivity solutions” aliongeza Karikari.

Tigo business inamiliki na kuendesha kituo cha data cha Kimataifa (Tier III Certified Data Center) Tanzania, kinachoruhusu kampuni za ndani kuhifadhi data zao na programu za biashara kwa usalama kupitia miundombinu iliyothibitishwa na mamlaka za kimataifa.

“Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye dunia ambayo taarifa au data zimepungua thamani hivyo zinahitaji kuhifadhiwa na kuchakatwa kwa ufanisi mkubwa ili kusaidia kampuni kufikia malengo ya biashara na ndiyo maana Tigo business imewekeza katika kuhakikisha inatoa suluhisho zenye kukidhi mahitaji na bajeti za kampuni,” alisema.

Kupitia miundombinu yenye usalama inatoa uhuru kwa wateja kuunganishwa na huduma za uhakika kupitia kwa watoa huduma wengine au moja kwa moja na Tigo na pia inatoa uhakika wa huduma kwa asilimia 99.982% hivyo kuzifanya biashara kuzalisha zaidi jambo linalochochea ukuaji wake.
Afisa Mkuu wa Tigo business, Pavan Ramdhani aliwaarifu wateja wa Tigo business wakati wa uzinduzi kuwa “Tovuti hii mpya itasaidia wamiliki wa makampuni kutumia muda mwingi katika biashara zao kwa kuwapa nafasi ya kujihudumia na kupata thamani halisi kupitia chaneli wanazopenda.Hii itawapa uwezo wateja na kutoa huduma bora kwa wateja wao,”

Aliogeza “Wateja wanaweza kusimamia akaunti zao, kuuliza na kupata ripoti ikiwamo za ankara pamoja na kupata huduma kwa wakati.Pia, tovuti inaruhusu wateja kusimamia na kudhibiti gharama za mawasiliano pamoja na kupanga rasilimali kwa watumiaji kulingana na mahitaji.Tovuti ni rahisi kutumika na inapatikana kupitia link https://tigobusiness.tigo.co.tz/Login/Tz.”
Tigo business inatoa suluhisho kwa biashara zote bila kujali ukubwa wake na kuzisaidia kampuni kujikita kwenye mambo ya msingi kwenye biashara kwa mustakabali wa baadaye. Tupigie 0711 100 101 au tutumie e-mail kupitia: tigobusiness@tigo.co.tz kupata huduma kwaajili ya biashara yako kwa gharama nafuu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post