RAIS MAGUFULI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI KUKOPA BENKI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, November 28, 2019

RAIS MAGUFULI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI KUKOPA BENKI

  Malunde       Thursday, November 28, 2019

Rais Magufuli amewapiga marufuku Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuacha  mara moja kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa madai ya kufanya miradi ya maendeleo.Ametoa kauli hiyo Jumatano Novemba 27, 2019 wilayani Bukombe mkoani Geita wakati akihutubia mkutano wa hadhara, Rais Magufuli amewaagiza iwapo wapo ambao wameshachukua fedha hizo kuzirudisha na kuvunja mikataba waliyoingia.

“Kama kuna mkurugenzi yeyote amekopa fedha azirudishe, mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya Serikali ni paymaster general wa Serikali ambaye ni Wizara ya Fedha pekee.”

“Anayekopa ajiandae kutoka. Naamini Wakurugenzi wamenielewa, nimepita Kahama Mkurugenzi ananiambia anataka kukopa kutoka TIB (Benki ya Uwekezaji Tanzania) kwa ajili ya kujenga stendi, haiwezekani fedha za wananchi kuchezewa, ovyo”  alisema Rais Magufuli
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post