MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2019 KUANZA KESHO


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles  Msonde amesema jumla watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 kati yao wa shule ni 433, 052 na 52, 814 wa kujitegemea.

Dk Msonde ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 wakati akizungumza kuhusu kuanza kwa mitihani hiyo kesho  katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kati ya watahiniwa 433,052 waliosajiliwa wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842.

Dk Msonde amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote za muhimu zinazohusu mchakato huo katika mikoa ya yote ya Tanzania Bara na Visiwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527