BODI YA MIKOPO HESLB YATOA ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO AWAMU YA TATU 2019/2020

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa orodha ya tatu ya  majina ya wanafunzi waliopata mkopo  yenye jumla ya wanafunzi 4785 wa mwaka wa kwanza wa masomo 2019/2020.

Wanafunzi hao wamepata mikopo yenye thamani ya Sh14.3 bilioni na hivyo kufanya idadi  ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo kufikia 46,838. yenye thamani ya sh162.86.

Taarifa iliyotolewa  Jumapili Novemba 3, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru imeeleza kuwa wanafunzi waliopata mikopo katika awamu ya tatu wanaweza kupata taarifa zao kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo


Kuhusu taratibu za malipo kwa wanafunzi, amesema fedha za wanafunzi waliopata mikopo zimeshapelekwa vyuoni na vyuo vimeelekezwa kuhakikisha fedha zinawafikia wanafunzi walengwa mara wanapofika na kukamilisha taratibu za usajili.

Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikali imetenga Sh450 bilioni kwa ajili ya wanafunzi 128,285. Kati yao, wanafunzi 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo ya mwaka wa pili, tatu na kuendelea.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527