MOTO WAUNGUZA NYUMBA NA KUUA WATU WANNE


WAKAZI wa Makueni, Bi Regina Mueni 49, binti yake Faith Mangeli na wajukuu zake Angel Masava na Amelina Masava wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto iliyoikumba nyumba yao iliyopo maeneo ya soko la Nyunzu maeneo ya Makueni nchini Kenya.

Katika tukio hilo mama yake Mueni aliyetambulika kwa jina la Monica Matolo, 75, alipata majeraha kadhaa ya moto na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya Makueni kwa ajili ya matibabu.


Aidha, katika uokozi huo mali za thamani zilishindwa kuokolewa na zikateketea. Taarifa zinaeleza kuwa nyumba hiyo ilikuwa na harufu kali ya petroli jambo linaloonyesha kuwa kuna mtu alihusika kuunguza nyumba hiyo.



Polisi wanamhisi kaka yake Mueni kuhusika katika tukio hilo kutokana na kuwapo kwa mgogoro wa ardhi wa kifamilia. Aidha, miili minne iliyokutwa katika tukio hilo ilibebwa na kwenda kuhifadhiwa mochwari ya hospitali ya rufaa ya Makueni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527