KUNDI LA IS LATANGAZA KIONGOZI MPYA ATAKAYEMRITHI ABU BAKR AL-BAGHDADI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 1, 2019

KUNDI LA IS LATANGAZA KIONGOZI MPYA ATAKAYEMRITHI ABU BAKR AL-BAGHDADI

  Malunde       Friday, November 1, 2019

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS limemtangaza kiongozi wake mpya baada ya kuthibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi katika shambulizi lililofanywa na Marekani nchini Syria. 

Taarifa iliyotolewa kwenye chombo cha habari cha IS, al-Furqan imeeleza kuwa nafasi ya al-Baghdadi itazibwa na Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi. 

Kundi la IS halikutoa taarifa zaidi kuhusu al-Qurayshi. Kiongozi huyo mpya anatambuliwa kama msomi, shujaa mashuhuri na kiongozi wa kivita ambaye amepambana na majeshi ya Marekani na ana ufahamu kuhusu vita hivyo. 

Taarifa hiyo pia imethibitisha kifo cha Abu Hassan al-Muhajir, msaidizi wa karibu wa al-Baghdadi ambaye alikuwa pia msemaji wa IS tangu mwaka 2016.

 Vifo hivyo ni pigo kubwa kwa kundi la Dola la Kiislamu karibu miezi saba tangu lilipofurumushwa kutoka kwenye ngome yake ya mwisho nchini Syria.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post