MKUU WA WILAYA YA TUNDURU, JULIUS MTATIRO ASIMAMIA ZOEZI LA WANAFUNZI WATORO KUCHAPWA VIBOKO MBELE YA WAZAZI WAO


Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro jana Alhamisi  alisimamia zoezi la  kucharazwa viboko wanafunzi 3 ambao ni watoro sugu katika Shule ya Msingi Ligoma iliyoko wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na utoro sugu, nidhamu za wanafunzi na mimba za utotoni Tunduru.


Mkuu huyo wa wilaya  alimtaka mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwachapa viboko vinne wanafunzi hao na kuagiza  wapewe adhabu nyingine zisizohusiana na viboko, ikiwa ni pamoja na kuchimba visiki.

Baada ya viboko hivyo, aliwauliza wanafunzi hao lini wataanza kwenda shule na mmoja alijibu kuwa ataripoti Jumatatu,hata hivyo, mkuu huyo wa Wilaya alisema wote wanapaswa kuripoti leo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post