JUMIA YAFUNGA BIASHARA ZAKE TANZANIA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 29, 2019

JUMIA YAFUNGA BIASHARA ZAKE TANZANIA

  Malunde       Friday, November 29, 2019

Mtandao wa biashara Barani Afrika umefunga biashara yake nchini Tanzani ikiwa ni siku chache tu baada ya kusitisha shughuli zake nchini Cameroon

Kulingana na taarifa iliyopatikana imeeleza kuwa Jumia imefunga shughuli zake nchini Tanzania ili kuwekeza rasilimali katika masoko mengine

Taarifa hiyo inasomeka: "Kwa kuzingatia tathmini yetu ya kuelekea mafanikio, tumefanya maamuzi magumu ya kusitisha shughuli zetu  Tanzania kuanzia Novemba 27, 2019.


"Tanzania kuna fursa kubwa lakini tumeona ni vyema kutumia rasilimali zetu katika masoko mengine, uamuzi huo sio rahisi lakini unatusaidia kuweka mkazo na rasilimali zetu mahali ambapo tunaweza  kuleta matunda na kusaidia ustawi wa Jumia"


Aidha, imesema itaendelea kutumia mtandao wake wa ''Jumia Deals'' katika kuendelea kuwasaidia maelfu ya wafanyabiashara ambao wanautumia kukutana na wanunuzi

Novemba 18, 2019 kampuni hiyo ambayo makao makuu yake yapo nchini Nigeria ilifunga biashara zake  nchini Cameroon kwa sababu kama hizo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post