HUMPHREY POLEPOLE AMPIGA KIJEMBE SUMAYE BAADA YA KUPIGWA CHINI UCHAGUZI CHADEMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amempiga  kijembe  Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye baada ya kubwagwa kwenye Uchaguzi wa Kikanda ndani ya CHADEMA.

“Nimesikia Mzee Sumaye hata Uenyekiti sijui wa “Kitongoji” wamembwaga huko Pwani, alipokuwa CCM @ccm_tanzania tulimpa kwa upendeleo Uwaziri Mkuu Miaka 10. Mzee, nadhani muda umefika huko hakuna watu, mimi na wewe tunajua imetosha. Mwenzio amepumzika na muda wa kulea wajukuu anao!” ameandika ujumbe huo katika akaunti yake ya Twitter.
Uchaguzi huo ulifanyija jana jioni Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye peke yake ndipo zikapigwa kura za ndio au hapana

Matokeo ya kura za ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48 .Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post