CDEA WAFANYA MAJADILIANO YA JIJI BUNIFU KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MIKOCHENI B


TAASISI ya Utamaduni na Maendeleo Afrika Mashariki (CDEA)  imeendesha majadiliano ya Jiji bunifu (Creative City Dialogue)  kwa wakazi na wafanyabiashara wa soko la Mikocheni B, Jijini Dar es Salaam.


Katika majadiliano hayo CDEA kwa kushirikiana na taasisi ya Zaidi Recyclers kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswis wameweza kuwafikia wananchi hao wa Mikocheni B  ambapo walijadili mada za urejelezaji (recycling) na fursa zake.

Awali akitambulisha mradi huo, Afisa mradi wa CDEA, Anjela Kilusungu alisema Urejelezaji (recycling)  una fursa nyingi hivyo wananchi wachangamkie fursa hizo.

“CDEA kwa kushirikiana na wadau wetu tumeona ni vyema kutoa taarifa za urejelezaji ambapo kupitia njia ya majadiliano itasaidia kufikisha elimu na kupambanua  kwa kina fursa zilizopo  kama kipato, uhifadhi wa mazingira na kuboresha afya” alisema Bi Angela Kilusungu.

Angela Kilusungu aliwaomba wakazi wa Mikocheni wakiwemo wafanyabiashara wa soko hilo la Mikocheni B, waanze kutenga taka kama njia ya kwanza kabisa ya shughuli ya urejelezaji  pamoja na kuwasihi kulitumia jalala lililopo katikati ya soko hilo kwa umakini ili liweze kuwa chanzo cha mapato katika soko hilo.

Kwa upande wake, Afisa Miradi wa Kampuni ya Zaidi recyclers Eva Msella aliweza kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao  namna utenganishaji wa taka, uhifadhi na urejelezaji unavyokuwa fursa.

Eva Msella alisema kwa sasa taka zina faida endapo zitatenganishwa na kurejelezwa kuwa bidhaa mpya ambapo pia amewaelezea wananchi hao juu ya fursa  ya taka ambazo zinaweza kuwaingizia kipato cha kuendesha maisha yao kwa kutengeneza taka hizo na kuwa bidhaa kama mbolea, mapambo na samani za majumbani.

Mjadara huo wa Jiji bunifu  upo chini ya mradi wa “Taka Yangu, Hazina Yangu” ulioendeshwa kwa miezi sita katika kusaidia kupunguza tatizo la taka ngumu zinazodhalishwa jijini Dar es Salaam kwa tutumia sanaa chini ya usimamizi wa CDEA  kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswis.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527