AWESO AWATAKA WENYEVITI WAPYA WA VIJIJI,VITONGOJI WASIGEUKE KUWA WAUZA ARDHI BADALA YAKE WAWATUMIKIE WANANCHI


 MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na Naibu Waziri wa Maji akizungumza  na wananchi Kata ya Kipumbwi wilayani humo ambapo aliwataka wenyeviti wapya kuhakikisha wanachochea kasi ya maendeleo kwa wananchi 

 MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza 
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia akizungumza kushoto  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah

 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza
 MBUNGE wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji  katika akikata utepe kushiria ufunguzi wa tawi la kikoba la Jipe Moyo la Pangani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Pangani Rajabu Abdallah
 MBUNGE wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji akicheza pamoja na wenyeviti wapya waliopita wilayani Pangani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wenyeviti wa Vijiji, vitongoji na mitaa waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita wasiwe chanzo cha migogoro kwa wananchi kwa kugeuka wauza ardhi bali wahakikishe wanashirikiana nao kutatua kero zinazowakabili.

Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji aliyasema  wakati mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani ambapo alisema lazima watambue dhamana kubwa walioibeba ni kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao.

Alisema kwamba wananchi wanataka maendeleo ndio maana wamewachagua hivyo wanajukumu kubwa la kutekeleza hayo kwa vitendo ikiwemo kutetea maslahi yao pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali.

“Unapokuwa kiongozi lazima utetee maslahi ya wananchi wako pia utembue changamoto zinazowakabili hapa kipoumbwi asilimia kubwa wananchi shughuli zao na uvuvi hivyo Mwenyeviti mpya wa hapa kuwa imara kusimamia wavuvi waweze kuvua kwa usalama wapate ridhiki yao ya halali”Alisema Aweso.

Mbunge huyo pia aliwaambie wananchi kwamba hakuna demokrasia yoyote ya kutafuta viongozi kwenye Taifa hili zaidi ya uchaguzi hivyo vikiwemo kuwataka iongozi ambao wamepatikana watambue kwamba wana kipumbwi na wana Pangani wanahitaji maendeleo na sio jambo jingine.

Hata hivyo pia aliwataka pia hakikisha kila baada ya miezi mitatu wanasoma mapato na matumizi huku akiwaambia kwamba sio wakati ukiwa umefika hata simu zao hazipatikani kwa kuwaeleza huo utakuwa sio uoingozi.

“Wapo watu wamewaaminisha watu kwamba CCM ikiingia hapa Kipumbwi watateseka hawataleta maendeleo…lakini wapo watu wanasema baada ya CCM kuingia hapa eti boti zitafukuzwa hafukuzwi mtu hapa “Alisema Mbunge huyo.

Mbunge huyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuwapa maendeleo wananchi hao maana hawana wenyeviuti wengine zaidi ya nyie.

“Eneo la Kipumbwi ni eneo lenye mapato makubwa watu wanataka kupata maendeleo leo sizije fedha zinakusanywa nyingi lakini hata choo  cha kujisaidia hakuna hakikisheni mnabadika sasa”Alisema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527