ALIYETAJWA NA RAIS MAGUFULI KUIBA SH MILIONI 7 KWA DAKIKA AACHIWA HURU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 16, 2019

ALIYETAJWA NA RAIS MAGUFULI KUIBA SH MILIONI 7 KWA DAKIKA AACHIWA HURU

  Malunde       Wednesday, October 16, 2019 Hatimaye mfanyabiashara Mohamed Yusufali, aliyekuwa akikabiliwa na kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi akidaiwa kukwepa kodi na kuisababishia Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh27 bilioni, katika kesi zote mbili yeye na wenzake, amerejea uraiani.


Yusufali ambaye aliwahi kutajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali Sh7 milioni kwa dakika kupitia mashine za kodi za kielektroniki (EFD), alirejea uraiani jana baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitatu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha.

Hivyo Yusufali aliachiwa jana rasmi baada ya kukamilisha mchakato wa msamaha wa Rais kisheria mahakamani, kwa mujibu wa makubaliano yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kesi ya pili iliyokuwa imebaki.


Na James Magai, Mwananchi


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post