TMA YATAHADHARISHA MVUA KUBWA KUNYESHA DAR,TANGA,PWANI,UNGUJA,PEMBA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 16, 2019

TMA YATAHADHARISHA MVUA KUBWA KUNYESHA DAR,TANGA,PWANI,UNGUJA,PEMBA

  Malunde       Wednesday, October 16, 2019


Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Dkt Agnes Kijazi

Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa siku mbili mfululizo, kuanzia Oktoba 17 na 18, 2019, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba, hali itakayopelekea kusimama kwa muda kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 16, 2019, na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwatahadharisha wananchi hususani waishio mabondeni, ambapo athari hizo pia zinaweza kujitokeza Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa upo uwezekano wa mvua hiyo kutokea kwa wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa usafiri.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post