TMA YATANGAZA MVUA KUBWA KUNYESHA KESHO DAR,TANGA,PWANI,ZANZIBAR,MORO


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kesho Jumamosi 5, 2019 katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 imeitaja mikoa mingine ni Pwani, Tanga, Zanzibar pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” imeeleza taarifa hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527