BIBI HARUSI AFARIKI 'AKIPIGA SELFIE' KWENYE BWAWA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 8, 2019

BIBI HARUSI AFARIKI 'AKIPIGA SELFIE' KWENYE BWAWA

  Malunde       Tuesday, October 8, 2019
Bibi harusi na watu wengine watatu wa familia yake wamekufa maji katika bwawa moja la maji baada ya kujaribu kupiga picha ya selfie, kulingana na maafisa wa polisi kutoka jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu.

Waliokufa ni miongoni mwa watu sita walioshikana mikono na kusimama katika kina cha maji marefu karibu na bwawa la Pambar kabla ya mmoja wao kuteleza, na kujaribu kumuokoa mwingine.

Mume wa mwanamke huyo aliweza kumuokoa dadaake lakini wengine wakafa maji. India ina idadi kubwa ya watu wanaofariki kutoka na vifo vya selfie.

India iliripoti vifo vya watu 259 kati ya 2011 na 2017 kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la maabara ya tiba nchini Marekani. Inafuatiwa na Urusi, Marekani na Pakistan

Katika jimbo la Tamil Nadu siku ya Jumapili . Wanandoa hao wachanga , kutoka eneo la Bargur katika eneo la Krishnagiri, walikuwa wakiwatembelea watu wa familia yao katika eneo la Uthangarai pamoja na dadake bwana harusi , kulingana na gazeti la Hindu.

Watatu hao waliingia katika maji hayo pamoja na vijana watatu wa familia moja , kabla ya mmoja wao mvulana mwenye umri wa miaka 14 kuteleza na kuwashika dada zake wawili mmoja wao akiwa na miaka 18 na mwengine wa miaka 19, pamoja na wanandoa hao wawili na dadake bwana harusi

Dada huyo alivutwa na nduguye lakini wengine wanne wakapotea ndani ya maji. Maafisa wa polisi wanasema kwamba miili yao baadaye ilipatikana na uchunguzi kufanywa.

Ni kisa cha hivi karibuni miongoni mwa msururu wa vile vya kupiga selfie nchini India. Wataalam walionya kwamba watu wanafanya hatari ili kuwafurahisha watu wa familia zao katika mitandao ya kijamii.

Katika jimbo la Haryana mnamo mwezi Mei , vijana watatu waliokuwa wakipiga picha za selfie katika reli waliruka kutoka katika njia ya barabara hiyo ya treni walipoona gari hilo likikaribia walikokuwa, kabla ya kuuawa na treni nyengie iliokuwa inajiri kutoka upande mwengine wa reli.

Mwaka 2017, Jimbo la India la Karnataka lilizindua kampeni ya kuwaonya watu kwamba selfie zinaweza kuua baada ya kifo cha wanafunzi wanne.

Mwaka huohuo, mtu mmoja alifariki katika eneo la Odisha wakati ndovu ambaye aliuwa akipiga selfie naye alimkamata na kumpiga na chini.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post