JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA SILAHA MBILI AINA YA SHORT GUN | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 19, 2019

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA SILAHA MBILI AINA YA SHORT GUN

  Malunde       Saturday, October 19, 2019
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata silaha mbili aina ya Short Gun zikiwa na risasi mbili ambazo zilikuwa kwenye mtutu wa kila silaha ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye mfuko wa plastiki.


Kufuatia msako mkali uliofanyika Oktoba 17, 2019 saa 17:00 jioni huko maeneo ya Pambogo, mtaa wa Isengo, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilikamata silaha hizo ambazo zimetengenezwa kienyeji na baada ya kuzikagua zilibainika kutokuwa na namba za usajili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ametoa  rai kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi cha watu ambacho wanakitilia mashaka katika maeneo yao ili ufuatiliaji ufanyike. 

Aidha ametoa rai kwa mtu yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hiyo mara moja kituo cha Polisi


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post