ALIYEKUWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO AHOJIWA TAKUKURU KWA UBADHIRIFU WA MILIONI 300 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 19, 2019

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO AHOJIWA TAKUKURU KWA UBADHIRIFU WA MILIONI 300

  Malunde       Saturday, October 19, 2019

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - Takukuru Mkoa wa Tanga inamhoji aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Kazimbaya Makwega kwa tuhuma za ubadhirifu wa Shilingi 300 milioni za upimaji wa viwanja katika shamba la Mnazi wilayani Lushoto.


Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba jana alisema Makwega alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya Mbozi kabla kutenguliwa na Rais John Magufuli.

Alisema zipo fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya upimaji wa viwanja na mkataba ulikuwa wa Sh300 milioni ambapo mtuhumiwa kwa kutumia nafasi yake anatuhumiwa kubadilisha baadhi ya vipengele.

Alivitaja vipengele vinavyodaiwa kubadilishwa mkurugenzi huyo ni vile vilivyoitaka Kampuni ya Geoplan (EA) ya jijini Dar es Salaam kuweka kiasi cha gharama kwa ajili ya tahadhari ikiwa itachelewa kukamilisha kazi ile gharama itakatwa.

Kamanda huyo wa Takukuru alisema mkataba huo wa upimaji ulitakiwa uanze Juni  28 mwaka 2013 hadi Agosti 28, 2018 kitu ambacho hakikufanyika hadi Desemba 3, 2018 ambapo muda ulikuwa  kinyume na taratibu za mkataba na hata fedha za dharura zilizotakiwa kukatwa kama kipengele cha 44 kinavyoonyesha hazikukatwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post