HARMONIZE, ALI KIBA WAMJIBU DIAMOND KUHUSU TAMASHA LAKE LA WASAFI FESTIVAL......." UNIKOME, UNANIIBIA PENSELI HALAFU UNANISAIDIA KUTAFUTA" | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 30, 2019

HARMONIZE, ALI KIBA WAMJIBU DIAMOND KUHUSU TAMASHA LAKE LA WASAFI FESTIVAL......." UNIKOME, UNANIIBIA PENSELI HALAFU UNANISAIDIA KUTAFUTA"

  Malunde       Wednesday, October 30, 2019
Muda mfupi baada ya msanii,  Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.


Kupitia mtandao wake wa Instagram, Ali Kiba ameandika; “Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME) Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz”

Leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019  jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.


Harmonize kwa upande wake alipoulizwa alijibu;  “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post