SIMBA YAPUNGUZIWA KASI SHINYANGA....YAPOKEA KICHAPO CHA WACHIMBA MADINI 'MWADUI FC'


Kikosi cha Simba kimeshindwa kutamba mbele ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Bao pekee la Wachimba Madini 'Mwadui FC' limewekwa kimiani na Gerald Mathias mnamo dakika ya 32 kipindi cha pili kwa njia ya kichwa.

Matokeo haya yanaifanya Simba ipoteze kwa mara ya kwanza msimu huu lakini ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama zake 18.


Matokeo kwa ujumla katika Ligi kuu Bara leo haya hapa

FT: Mwadui FC 1-0 Simba SC (Gerald Mathias 32')

FT: Ruvu Shooting 1-0 KMC (Santos Mazengo 17’) 

FT: Kagera Sugar 2-0 Namungo FC (Frank Ikobela 12’, Yusuphu Mhilu 69’) 

FT: Mtibwa Sugar 2-1 Coastal Union (Dickson Mbekya 20’, Jaffary Kibaya 56’ : Dickson Daud OG) 

FT: Lipuli FC 2-1 Polisi Tanzania (Kenneth Masumbuko 34’, Paul Nonga 74’  : Mohamed Mkopi 73’)

FT: Singida United 1-2 JKT Tanzania (Ramadhan Hashim 55’ : Danny Lyanga 36’, Adam Adam 41’)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527