WAZIRI KALEMANI AKUNWA NA KASI YA UJENZI MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE (JNHPP) WA MTO RUFIJI


 WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akitoa tathmini yake mbele ya sehemu ya kuingilia kwenye handaki la kuchepusha maji (diversion channel) la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji Mkoani Pwani leo Jumapili Septemba 8, 2019 wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme wa Megawati 2115


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KASI ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo leo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel) ikiwa imekamilika.
“Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.
Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.
Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji (diversion tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na ikamilike umbali wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.
“Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu kwamba watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri wataukab idhi na mimi niukabidhi kwa Watanzania na asitokee mtu atakaejaribu kuuchelkewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo.” Alionya.
Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi w aShirika la Umeme Nchini (TANESCO) alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.
 Daraja namba mbili  la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika leo Jumapili Septemba 8, 2019.
 Kijiko kikitoka kwenye handaki la kuchepusha maji leo Septemba 8, 2019.
 Waziri Dkt. Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali kwenye eneo la mradi
Msafara wa magari ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ukipita kwenye daraja namba mbili linalokatisha mto Rufiji leo Septemba 8, 2019.
Waziri Mhe. Dkt. Kalemani (katikati) akipatiwa maelezo na Mratibu wa mradi huo Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara 
Ujenzi wa nguzo za daraja namba moja litakalounganisha pande mbili za mto Rufiji ukiwa unaendelea. Daraja hilo litasaidia kuvusha vifaa vya ujenzi (mashine) kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili ili kusaidiana na daraja namba mbili ambalo tayari linafanya kazi.
Eneo la kuingilia ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Dkt. Kalemani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephene Kebwe na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Rufiji (OCD) Lepold Fungu, akipatiwa maelezo na Mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.
Mhe. Dkt. Kalemani akimsikilzia Meneja Mradi kutoka kampuni ya Arab Contractor ya Misri, Mhandisi Mohammad Samaha.(kushoto). 
Daraja namba mbili likiwa limekamilika na kufanya kazi
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (JNHPP), ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Steven Manda, mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post