MWALIMU AMCHARANGA PANGA MPENZI WAKE WAKIWA GESTI OLD SHINYANGAKamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard AbwaoNa Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanamke aitwae Neema Kabulu (19) amenusurika kufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni, tumboni,mkononi na Mwalimu Joseph Msafiri wa Shule ya Msingi Namagubu iliyoko Ukerewe Mkoani Mwanza ambaye ni mpenzi wake. 

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao kwa vyombo vya habari,tukio hilo limetokea Septemba 6,2019 majira ya saa nne kamili usiku katika maeneo ya Old Shinyanga, Kata ya Old Shinyanga, Tarafa ya Shinyanga Mjini, Manispaa ya Shinyanga.

"Neema Kabulu mkazi wa Ukerewe mkoani Mwanza alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni, tumboni na mkono wa kulia na Joseph Msafiri ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Namagubu iliyoko ukerewe Mkoani Mwanza, ambaye ni mpenzi wake",ameeleza Kamanda Abwao.

"Mwanaume Joseph Msafiri kwao ni Iselamagazi halmashauri ya Shinyanga,alimwambia mpenzi wake anakuja kumtambulisha ukweni, walilala guest Old Shinyanga na kesho yake ndiyo yalitokea hayo majanga, eneo la tukio tulipata panga lililotumika, na nguo zenye damu",amesema Kamanda.

"Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi. Majeruhi anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya. Mtuhumiwa amekamatwa",ameongeza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post