SPIKA NDUGAI AWAPONGEZA NAPE NNAUYE, JANUARY MAKAMBA NA WILLIAM NGELEJA KWA KUMUOMBA MSAMAHA RAIS MAGUFULI

Spika wa Bunge Job Ndugai, amewapongeza wabunge watatu wa CCM, Mh. Nape Nnauye, January Makamba na William Ngeleja kwa kitendo cha kiungwana cha kumuomba msamaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

 
Mh. Job Ndugai amesema Bungeni, leo September 12, 2019, kuwa ni vyema viongozi wote wakafuata nyayo hizo kwa wale wote ambao wamekuwa wakiwakosea hata kama ni wadogo kwako kicheo, kwakuwa uungwana ni vitendo.

Amesema anashangaa kuona magazeti mengi yamekuwa yakishabikia, na kuwachora wabunge picha za ajabu ajabu pamoja na kuandika habari za kishabiki baadhi ya vingozi nchini.

Pia amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwasemehe wabunge hao kwakuwa ni jambo la kiungwana sana kufanya kama binadamu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527