WATUMISHI WA UMMA 46 WAFUKUZWA KAZI KWA KUGHUSHI VYETI VYA TAALUMA MSALALA

NA SALVATORY NTANDU
Baraza la Madiwani la halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga limewafukuza kazi watumishi 46 waliojipatia kazi kwa njia ya udanganyifu kwa kughushi vyeti vya taaluma na kuisababishia serikali hasara.


Uamuzi huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu kwenye kikao cha kawaida cha kufunga mwaka wa fedha wa 2018/19 kilichofanyika jana katika makao makuu ya halmashauri hiyo.

Amesema watumishi hao walibainika katika zoezi la uhakiki watumishi hewa ambalo lilifanyika nchi nzima mwanzoni mwa mwaka 2014 na idara zilizobainika kuwa na watumishi wengini ni idara ya afya na Maji.

Amefafanua kuwa watumishi hao walighushi vyeti na kujipatia ajira hizo kinyume na sheria za Utumishi wa Umma na kuisababishia serikali hasara huku wajijua wazimkuwa ni kosa.

Mibako amesema baada ya kuchukua hatua hizo baraza liliandikia wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuhusu suala hilo ambapo hatua za haraka zilichukuliwa na tayari imeshaanza kuleta watumishi katika idara hizo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post