WATOTO 714,741 KUPATIWA CHANJO YA SURUA - RUBELLA NA POLIO KAGERA....UZINDUZI KUFANYIKA SEPTEMBA 26 - 30 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 19, 2019

WATOTO 714,741 KUPATIWA CHANJO YA SURUA - RUBELLA NA POLIO KAGERA....UZINDUZI KUFANYIKA SEPTEMBA 26 - 30

  Malunde       Thursday, September 19, 2019

Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa  wa Kagera Diocles Mjwahuzi akizungumza na waandishi wa habari

Na Lydia Lugakila- Malunde 1 blog
Jumla ya Watoto 714,741 kutoka katika Halmashauri 8 za mkoa wa  Kagera wanatarajwa kunufaika na chanjo ya Surua –Rubella na chanjo ya polio ya Sindano ili kuondokana vifo vitokanavyo na udumavu wa akili, utapiamlo na kupooza kwa viungo vya mwili.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 19, 2019 na Mratibu wa Huduma za chanjo mkoa wa Kagera Diocles Mujwahuzi katika Semina ya waandishi habari Mkoani Kagera katika kuelekea Kampeni shirikishi ya Surua –rubella na chanjo ya polio ya sindano kwa watoto hao walengwa.

Mjwahuzi amesema watoto walengwa wa chanjo Surua –Rubella ni 486,675 na chanjo ya chanjo ya polio ya sindano 228,066 wanakamilisha jumla ya laki 714, 741.

Amesema umri wa watoto hao wanaotarajiwa kupata chanjo hizo hizo ni kuanzia miezi 9-miezi 59 na kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka 3 na nusu .

Amesema jamii imekuwa haina mwamuko katika kuwapeleka watoto wao kupata chanjo jambo linalosababisha hatari ya watoto wasiopata chanjo kuwa chanzo cha maambukizi kwa watoto wengine ikiwemo udumavu wa akili, utapiamlo hadi kifo.

Amesema kampini hiyo inatarajia kuzinduliwa Septemba 26-30 mwaka huu na imelenga kuwafikia watoto ambao hawakupata chanjo kabisa na wale ambao walipata lakini hawakukamilisha hivyo amewahimiza wana habari kutumia kampini hiyo vyema ili kuhakikisha watoto walengwa wanapatiwa chanjo hizo.

Awali akifungua semina hiyo kwa waandishi wa habari Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dorosella Mjunwa amesema magonjwa ya Polio, Surua – Rubella yanawaathiri watu wazima huku watoto chini ya miaka 5 wakipata madhara makubwa zaidi

Amewahimiza akina mama kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto kupata chanjo hizo na kuodokana na dhana ya kuwa chanjo zina madhara.

Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa huduma ya Chanjo mkoa wa Kagera Gerase Ishengoma amesema magonjwa ya surua-Rubella yanaenezwa kwa njia hewa ambapo kwa upande wa polio ni kwa njia ya kula au kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye vidudu vya polio,

"Nawaomba sana wazazi na walezi leteni watoto katika vituo vya afya kila Halmashauri imetengewa vituo vya kutolea hizo huduma pamoja na vituo vilivyokuwepo tangu awali vitaendelea kutoa huduma hiyo",alisema

Wahudumu hao wamesema watakapofanikiwa kuyatokomeza kabisa magonjwa hayo watafanya ufuatiliaji wa wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma na kuhakikisha sampuri inapelekwa wizara ya Afya ili kujiridhisha kwamba katika jamii ya mkoa wa kagera hakuna ugonjwa wa kupooza.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Kagera Dorosella Mkubwa akitoa akizungumza  wakati wa ufunguzi wa  Semina ya waandishi habari Mkoani Kagera katika kuelekea Kampeni shirikishi ya Surua –rubella na chanjo ya polio ya sindano  kwa watoto hao walengwa.Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa  wa Kagera Diocles Mjwahuzi akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kagera leo.
Gerase Ishengoma Mratibu msaidizi wa huduma za chanjo mkoa wa Kagera akizungumza na waandishi wa habari
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post