Makubwa Haya : WANAWAKE WAWILI WABADILISHANA WAUME ZAO BAADA YA KUCHEPUKIANA

Wanawake wawili kutoka kaunti ya Busia, magharibi mwa Kenya wamewaacha watu na bumbuwazi mara baada ya kubadilishana waume zao kwa lengo la kutafuta furaha.

Lilian Weta mwenye umri wa 28, mama wa watoto watatu na Millicent Auma mwenye umri wa miaka 29, mwenye watoto wawili wamezua gumzo katika mtandao nchini Kenya kwa kuonekana kuwa wamefanya jambo la ajabu sana kwa wanandoa hao kuamua kubadilishana wenza.

Wiki moja iliyopita wapenzi hao waliandikishiana serikalini namna watoto watalindwa baada ya wanawake hao kubadilishana waume zao pamoja na watoto.
Wanawake hao wanadai walifikia maamuzi hayo baada ya kusukumwa na ugomvi usioisha katika familia zao.

Vyombo vya habari vya Kenya vimemripoti Lilian akisema alifikia uamuzi huo mara baada ya mume wake kumleta mwanamke mwingine katika nyumba yao ,mwezi mmoja uliopita.

"Mume wangu alinidanganya kuwa binamu yake kutoka Bungoma anakuja kututembelea hivyo niandae chakula, na sehemu ya kulala mgeni. Muda mfupi tu ulipita kuna mwanamke aliingia na kuniambia nimuachie nafasi kwa sababu hiyo ni nyumba yake sasa au anidunge kisu," Lilian alisema.

Lilian aliendelea kusimulia kuwa Auma alimwambia akamtafute mume wake na akimpata aoleke huko na kweli alimtafuta mume wa Millecent na kwenda kufunga ndoa halali wiki tatu zilizopita.

"Mwanamke huyu alikuja akilia na kulalamika kuwa mke wangu amemchukua mume wake na nyumba yake,"

"Nilimwambia kwamba kama mke wangu ndio amekufukuza kwako basi nenda ukachukue mizigo yako na watoto na uje ukae na mimi hapa," alisema Bwire ambaye alikuwa mume wa Millecent.

Ni wiki mbili sasa Lilian Weta alipoolewa na Christopher Bwire baada ya wapenzi wao kuwasaliti na wanadai kuwa hawajutii kitendo walichokifanya.

Bwire ameviambia vyombo vya habari nchini humo jinsi maisha yake yalivyobadilika na kuwa ya furaha.

"Wabaya wawili wapatane na wawili wazuri wapatane, sina msongo wa mawazo.

Siku hizi ninaamka muda ninaotaka na kulala muda ninaotaka ninakula vizuri, nina furaha sana kuwa na Lilian," alisema Bwire.

Na upande wake Lilian pia anadai kuwa ana furaha sana kukaa na Bwire.

Barasa ambaye ni mume wake Lilian zamani anasema kuwa hana haja ya kumfuata mke wake na hataki kujua chochote kumuhusu kwa sababu yeye na Auma wana furaha sana.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527