EVANS AVEVA NA KABURU WAONDOLEWA MASHITAKA YA UTAKATISHAJI FEDHA.....MAHAKAMA YASEMA DHAMANA YAO IKO WAZI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.


Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 8 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zachariah Hans Pope.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni la upande wa mashitaka, pia kwa kosa moja moja na sio kwa kutegemeana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527