Breakinga : AJALI YAUA ASKARI WA JWTZ WAWILI KIGOMA

Na Editha Karlo - Malunde1 blog 
ASKARI wawili wa Jeshi la wananchi(JWTZ) kikosi cha 24KJ Mkoani Kigoma,wamefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika ajali  iliyotokea leo kwenye  hifadhi ya Katavi.


Askari hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi  lililokuwa limebeba silaha kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni Mkoani Katavi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni Lameck Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi hao pamoja na maiti mbili.

"Ilikuwa majira ya saa 8 tulipokea majeruhi 20 na wawili wakiwa wamefariki dunia ambao tumewapatia  huduma ya kwanza,wapo waovunjika mikono na miguu pia lakini tunafanya utaratibu kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili au Bugando",alisema.

Aliwataja waliofariki  ni Bakari juma Mohamed,Rashid Abed Mwimbe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527