ZIMBABWE YAPINGA TAMKO LA NCHI ZA ULAYA....YASEMA KAMWE HAITARUHUSU TISHIO LA MAPINDUZI LINALOTOLEWA NA UPINZANI

Serikali ya Zimbabwe imesema, haitaruhusu tishio lolote linalotolewa na upande wa upinzani la kupindua serikali, huku ikisisitiza kwamba raia wana haki ya kikatiba lakini hawapaswi kukiuka haki za wengine.




Tamko hilo la serikali limekuja baada ya Umoja wa Ulaya na nchi nyingine za magharibi zikiwemo Uingereza na Marekani kutoa taarifa ya pamoja hapo jana, ikiilaumu serikali ya Zimbabwe kwa madai ya kukiuka haki za binadamu wakati wa maandamano yaliyoongozwa na kundi la upinzani huko Harare tarehe 16 mwezi huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527