ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS ZIMBABWE AKIMBILIA MAFICHONI KUKWEPA KUKAMATWA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 21, 2019

ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS ZIMBABWE AKIMBILIA MAFICHONI KUKWEPA KUKAMATWA

  Malunde       Wednesday, August 21, 2019

Makamu wa Rais wa zamani wa Zimbabwe ametangazwa na mamlaka nchini humo kama Mhalifu aliyekimbia.

Gazeti linalomilikiwa na serikali la Herald limesema kwamba Phelekezela Mphoko amekimbia kukamatwa na Kamisheni ya kupambana na rushwa nchini humo, ZACC.

Kiongozi huyo aliyekua madarakani mwaka 2014 hadi 2017 amekua akitafutwa ili kufunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi pamoja na rushwa. 

Aliwahi pia kua balozi akiwakilisha Zimbabwe nchini Afrika ya Kusini, Botswana pamoja na Urusi

Wakili wa kiongozi huyo, Zibusiso Ncube alisema mteja wake alitoweka baada ya kuhofia kukamatwa na kuwekewa sumu.

Inaelezwa kuwa makamu huyo alikuwa sehemu ya kikundi ambacho kilitaka Neema ambaye ni mke wa Rais Mugabe afanikiwe badala ya Mnangagwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post