JE NI KWELI YESU FEKI ALIYEIBUKIA KENYA NA KUZUA GUMZO AMEFARIKI DUNIA???


Michael Job akiwa anaongea nchini Kenya.

Michael Job, muhubiri wa Marekani na muigizaji ambaye hivi majuzi alizuru Kenya na kuitwa 'Yesu bandia' hajafariki kama ilivyoangaziwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na Kenya.

Kulingana na uchunguzi wetu jamaa huyo yupo hai na mzima kama kigongo.
Kadhalika, muhubiri huyo yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa na vyombo hivyo vya habari.

Taarifa za vyombo hivyo ambazo zilianza kuenezwa siku tano zilizopita zinadai, Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini.

Ilidaiwa kuwa Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527