Picha : MZUNGU ALIYEDHANIWA KUWA NI 'YESU WA KISASA' AZUA GUMZO


Mnamo Jumatano, Julai 24, 2019 mtaa wa Kitengela  jijini Nairobi nchini Kenya ulikuwa umejawa na furaha tele pamoja na nderemo huku mzungu aliyekuwa amevalia mavazi ya kidini akipita. 


Michael Job, mhubiri kutoka Marekani alikuwa amevalia mavazi yake ya kuigiza huku akiwa ameachilia nywele zake. 

Nairobi Karibia waumini wote walikuwa na furaha ya kumuona mwanaume huyo aliyedhaniwa kuwa ndiye Yesu wa kisasa huku akitembea kwa madaha na kuzungumza kwa ujasiri mkubwa.

 Hata hivyo, licha ya wengi wao kumfahamu kuhusiana na mahubiri yake hakuna aliyekuwa akimtambua zaidi. 

Wakati mwingine huvalia mavazi ya kawaida na kupiga picha tu kama watu wengine.

 Kwa mujibu wa picha zake ni ishara tosha kuwa ni mtu ambaye anapenda kusafiri sana na kukutana na watu kutoka tabaka mbalimbali. Mhubiri huyo pia huwa na utani.

Japo ulidhania mhubiri huyo hushinda amevalia mavazi yake ya uigizaji basi sio hivyo kulingana na picha zake. 

Mugizaji huyo alikuwa miongoni mwa wahubiri walioalikwa kuidhinisha misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo kwa jina Kiserian Mega Interdenominational.

Badala ya kuendesha punda, alikuwa akitimbelea kwa gari la kifahari akiwa chini ya ulinzi mkali huku akiwatazama wakazi hao wenye furaha akiwa juu ya gari.

 Bado baadhi ya watu wamesalia na maswali ya mbona mhubiri huyo alikuwa akisisitiza kuitwa ' Yesu Kristu wa kisasa. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527