WATATU WASHITAKIWA KWA MAUAJI YA MWANAMKE WA MIAKA 55 WAKIMTUHUMU NI MCHAWI


Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora limewakamata Watu watatu na kuwafikisha Mahakama ya Wilaya ya Igunga   kwa tuhuma za mauaji ya Mama wa miaka 55, Veronica Makumbi, baada ya kumtuhumu kuwa ni Mchawi


Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua mwanamke huyo July 28 mwaka huu saa 6:30 usiku.

Waliokamatwa ni Sung'hwa Ngasa, Willson Sunhnwa na Sunhwa Zumbi wakazi wa kitangili.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elimajid Kweyamba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Igunga, Lydia Ilunda, alidai washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002. 

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29, itakapotajwa tena na washtakiwa walipelekwa mahabusu na hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo..


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527