Picha : MKUU WA MKOA WA KAGERA AVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KUFANIKISHA WIKI YA UWEKEZAJI KAGERA


Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akimkabidhi cheti cha pongezi mwandishi wa habari wa Malunde 1 Blog Lydia Lugakila kwa kazi nzuri aliyoifanya kutangaza fursa za uwekezaji mkoani Kagera wakati wa Wiki ya Uwekezaji Kagera iliyofanyika kuanzia Agosti 12,2019 hadi Agosti 17,2019.
****

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amevipongeza vyombo vya habari mkoani Kagera ikiwemo Malunde 1 Blog kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii iliyowafanya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuzitambua na kuzijua fursa mbalimbali  za uwekezaji zilizopo mkoani Kagera.Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa pongezi hizo leo Agosti 29,2019 wakati wa  mkutano maalumu na waandishi wa habari uliolenga kuwapongeza waandishi wa habari mkoani Kagera kwa kazi nzuri walizofanya kuutangaza mkoa wa Kagera wakati wa Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera iliyofanyika kuanzia Agosti 12,2019 hadi Agosti 17,2019.

Mkuu huyo wa mkoa amesema anatambua kazi nzuri wanayoifanya waandishi wa habari mkoani Kagera na wamekuwa na ushirikiano mkubwa hasa katika kipindi cha Wiki ya Uwekezaji Kagera ambapo wamezitangaza fursa zilizopo mkoani humo.

"Natumia fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza Wana habari mkoani hapa,mmefanya kazi usiku na mchana kuutangaza mkoa wetu, baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza matangazo ya moja kwa moja bure, bila gharama yoyote.Ninawashukuru sana naomba tuendelee kushirikiana ili kuwaletea maendeleo wananchi",amesema Gaguti.

"Sekta ya Habari ni sekta muhimu kwani kazi wanayoifanya ni ngumu na inayoleta manufaa makubwa katika jamii,tutaendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa wana habari kwani tayari milango imefunguliwa mkoani hapa".

Kwa upande wake Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Kagera Phinias Bashaya amempongeza mkuu wa mkoa, kwa ushirikiano mzuri anaotoa kwa kwa vyombo vya habari huku akimuahidi kuwa waandishi wa habari wataendelea kushirikiana naye kufanya kazi nzuri itakayojenga jamii imara na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akizungumza katika mkutano maalumu na waandishi wa habari mkoani Kagera ambapo amevipongeza vyombo vya habari mkoani Kagera ikiwemo Malunde 1 Blog kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii iliyowafanya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuzitambua na kuzijua fursa mbalimbali  za uwekezaji zilizopo mkoani Kagera.
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Kagera Phinias Bashaya akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kwa ushirikiano mzuri anaotoa kwa kwa vyombo vya habari mkoani Kagera.


Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akimkabidhi cheti cha pongezi mwandishi wa habari wa Malunde1 Blog Lydia Lugakila kwa kazi nzuri aliyoifanya kutangaza fursa za uwekezaji mkoani Kagera wakati wa Wiki ya Uwekezaji Kagera iliyofanyika kuanzia Agosti 12,2019 hadi Agosti 17,2019.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti  akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti  akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti  akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Kagera.
SOMA HABARI KUHUSU WIKI YA UWEKEZAJI KAGERA <HAPA>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post