PROFESSOR J NA PRODUCER P-FUNK MAJANI 'WATEMEANA CHECHE' MITANDAONI


Rapa maarufu hapa  nchini ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay’,   ameibuka na kuikanusha vikali taarifa ya Chama cha Hakimiliki Tanzania (The Copyright Society of Tanzania – COSOTA) kwamba wamemsimamia na kuhakikisha  amelipwa pesa zake Tsh. milioni 100, kutoka nchini Uganda.



Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Prof. Jay amewataka COSOTA kuweka rekodi sawa kwani hajapewa pesa hizo yeye, bali alilipwa mwandaaji wa kazi za muziki, prodyuza Majani ‘P Funk’, kwa kutumia ‘melody’ ya wimbo wa NIKUSAIDIEJE ulioimbwa na Prof J na Majani akiwa prodyuza.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Prof Jay, P Funk  Majani  alionekana  kupandwa na hasira na kuamua kumpa Makavu Prof. Jay kwa kudai kuwa ni mlafi na anaroho mbaya.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527