DC MBONEKO AWAAGIZA MAOFISA KILIMO KUACHIA VITI MAOFISINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko

Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ambapo amewaagiza maofisa kilimo kuacha tabia ya kukaa maofisini bali waanze kutembelea wakulima, na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa kuanzia maandalizi ya shamba hadi mavuno.

Akizungumza wakati wa ziara yake leo Agosti 29,2019 kwenye kijiji cha Manyada kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, mkutano uliofanyika kwenye jengo la Zahanati ya kijiji hicho ameagiza maofisa kilimo wote kuacha tabia ya kukaa maofisini.

Amesema hivi sasa wakulima wanapaswa kuanza kupewa elimu ya maandalizi msimu ujao wa kilimo, kuanzia namna ya kupata mbegu bora, kuandaa mashamba, madawa mazuri ambayo watatumia, pamoja na kulima kilimo cha kisasa chenye tija, ambacho kitawapatia mavuno mengi na kuinuka kiuchumi.

“Naagiza maofisa kilimo wote wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, acheni tabia ya kukaa maofisini, bali tembeleeni wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa chenye tija, kuanzia maandalizi ya shamba, pembejeo bora ambazo watazitumia hadi mavuno, ikiwa tunataka wakulima wanufaike na kilimo chao kuinuka kiuchumi,”amesema Mboneko.

“Pia nawaomba wakulima wa zao la pamba, mrudishe fedha za Pembejeo ambazo mlikopeshwa kwenye msimu wa kilimo uliopita, ili Serikali ipate fedha za kununua Pembejeo zingine ambazo zitawasaidia kwenye msimu ujao wa kilimo,”ameongeza.

Katika hatua nyingine amewapongeza wananchi wa kijiji hicho cha Manyada, kwa kujenga jengo la zahanati kwa nguvu zao wenyewe, ambalo limeshapauliwa na kuwataka wananchi waendelee kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo akibainisha kuwa, Serikali itawaunga mkono kukamilisha miradi hiyo.

Naye mtendaji wa kijiji cha Manyada John Clement, akisoma taarifa ya kijiji ametaja changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa kijiji hicho kuwa ni kutokamilika ujenzi wa Zahanati, umeme wa REA kutoenea maeneo yote, pamoja na ubovu wa barabara.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Manyada wamepongeza ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ambayo imewapatia matumaini ya kutatuliwa kero zao, zikiwamo za miradi ya maji, barabara, umeme, elimu, pamoja na afya.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua na kuwaagiza maofisa kilimo watembelee wakulima na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa kuanzia ngazi ya maandalizi ya mashamba. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi wa Kijiji cha Manyada kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na kuwapongeza kwa kujenga Zahanati ya kijiji hicho kwa nguvu zao wenyewe. Aidha akiwataka wazazi kupenda kusomesha watoto wao na kuacha tabia ya kuwaozesha ndoa za utotoni, ili wapate kutimiza malengo yao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi wa kijiji cha Manyada kuacha tabia ya kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo, huku akiagiza pia viongozi wa kijiji kujenga tabia ya kusoma mapato na matumizi.

Mtendaji wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, John Clement akisoma taarifa ya kijiji hicho, na kuelezea kuwepo na changamoto ya ukamilishwaji wa jengo la zahanati, miundombinu mibovu ya barabara, umeme, pamoja na ukosefu wa maji safi na salama hasa kutoka Ziwa Victoria.

Mwananchi John Joshua akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero zao na kuzitatua na kuuliza juu ya upatikanaji wa maji safi salama hasa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na kuondokana na matumizi ya kutumia maji yasiyo salama.

Mwananchi John Daniel akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko na kuhoji juu ya fedha za ahadi za Rais John Magufuli shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji.

Mwananchi Lukuliko Shija akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko juu ya sekta ya elimu, ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya msingi Manyada.

Mwananchi Terezia Bundala, akiuliza swali kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, juu ya ukamilishwaji wa Zahanati ya kijiji hicho ili ipate kuwasaidia kimatibabu na kuondokana na umbali mrefu wa kufuata huduma za afya.

Diwani wa kata ya Usanda ,Mhe. Forest Nkole akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Mtendaji wa Kata ya Usanda Emmanuel Maduhu akijibu swali la gharama za ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ambalo liliulizwa na wananchi na kujibu imeshatumia fedha za Serikali Shilingi Milioni 18.5 ukitoa nguvu za wananchi na hadi kukamilika kwake zinahitajika zaidi ya Shilingi Milioni 40.

Kaimu Meneja Wakala wa Maji Safi Vijijini (RUWASA) Alfred Pesa akijibu maswali ya miradi ya maji ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Dkt. Joseph Ngowi akimwakilisha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akijibu maswali ya idara ya afya ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Msimamizi wa umeme Vijijini (REA),Helly Twaha ambaye ni  akimwakilisha meneja wa Tanesco mkoa wa Shinyanga, akijibu maswali ya umeme ambayo yameulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

 Mkuu wa idara ya ardhi,Thomas Tukay akimwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Manyada kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, pamoja na baadhi ya wataalamu,wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Awali Mtendaji wa Kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Emmanuel Maduhu(kushoto) akimwelezea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko namna wananchi walivyojitolea kujenga Zahanati ya kijiji hicho na hatua walipofikia.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Manyada ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi likiwa limepasuka nyufa mara baada ya tetemeko la ardhi kupita eneo hilo,  kushoto ni Dkt. Joseph Ngowi akimwakilisha mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiwa msibani na kutoa salamu za pole kwa diwani wa Kata ya Mwamala Hamisi Masanja, ambaye amefiwa na mtoto wa kaka yake, ambapo awali ilikuwa afanye mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, lakini baada ya kukuta msiba ilibidi aahirishe mkutano huo na kwenda msibani.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post