RAIS ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


Rais Félix Tshisekedi ametangaza baraza jipya la mawaziri katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya kwanza ya rais Félix Tshisekedi imetangazwa leo Kinshasa, baada ya kusubiriwa kwa miezi saba.

Katika serkali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia kumi na saba ya mawiziri na wanaume asilimia 83.

Mnamo Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano.

Walikubali kuunda serikali itakayo kuwa na mawaziri 66.

Kama walivyo kubaliana, chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527