TANZANIA YAMWAGIWA SIFA KWA KUWA NCHI PEKEE YA SADC AMBAYO UCHUMI WAKE UNAKUA KWA ASILIMIA 7

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC  Dr. Stergomena Lawrence Tax ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.



Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.


 "Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze." Amesema Dr Tax na kuongeza;


"Katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda  hata Tanzania ,  tumeona mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea"


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527