POLISI WAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE....KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA ACT- WAZALENDO ACHUKULIWA KWA MAHOJIANO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 16, 2019

POLISI WAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE....KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA ACT- WAZALENDO ACHUKULIWA KWA MAHOJIANO

  Malunde       Friday, August 16, 2019

Katibu wa  Itikadi na Uenezi wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu  amechukuliwa  na Jeshi la Polisi kwa Mahojiano  alipokuwa katika Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es salaam  akiandaa mkutano wa kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzungumza na waandishi habari.

Jeshi la Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam lilifika katika makao makuu ya chama hicho  na kuzuia  mkutano  huo ambao ulitarajiwa kufanyika leo Ijumaa Agosti 16,2019 saa 5 asubuhi.

Polisi waliwasili Makao Makuu ya chama hicho  na kumhitaji kiongozi yoyote wa chama baada ya kumkosa Zitto Kabwe.

"Ndugu waandishi huu mkutano usubiri kwanza, kwa hiyo ninawaomba mtawanyike mara moja," alisema askari mmoja.

Wakati waandishi wakitawanyika aliwasili Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ambaye walimchukua  na kuondoka  naye kwa ajili ya mahojiano.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post