MBARONI KWA KUMUUA MUME WAKE KWA BISIBISI

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MWAJUMA Omary Malembeka (28)anadaiwa kumuua mume wake Selemani Kondo (43) mkulima na mkazi wa Chamalale,kata ya Vihingo,Mzenga ,wilayani Kisarawe mkoani Pwani, kwa kumchoma na bisibisi kwenye bega.


Akithibitisha kuhusu tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani hapo, Wankyo Nyigesa alisema mwanamke huyo alifanya maamuzi hayo kutokana na wivu wa kimapenzi.

Alieleza, kulikuwa na mzozo baina yao ambapo Mwajuma alimtuhumu mume wake kuwa siyo mwaminifu katika ndoa yao.

“Selemani aliuawa kwa kuchomwa bisibisi katika bega lake la kushoto na sehemu ya juu na mke wake huyo”alifafanua.

Wankyo alisema, kujichukulia sheria mkononi sio jambo la msingi kwani inaweza kuleta madhara kama ya kujeruhi ama kusababisha kifo ,na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Katika hatua nyingine, huko kijiji cha Lulenga, Ubena ,jimbo la Chalinze polisi walimkamata Kitenye Lumange ,mfugaji wa jamii ya kimasai (24) kwa kosa la wizi wa ng’ombe 13 wenye thamani ya sh.milioni 7.2 mali ya Arisen Hussein mkazi wa kijiji cha Visakazi .

Kamanda huyo alibainisha,wanawasaka watuhumiwa wengine walioshiriki kuiba mifugo hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527