MASHAMBULIZI MAWILI YA RISASI OHAIO NA TEXAS NCHINI MAREKANI YAUA WATU 30

Watu kumi wameuawa kufuatia shambulizi la risasi katika mji wa Dayton, Ohio nchini Marekani. 


Polisi wamesema hayo mapema jana Jumapili na kuongeza kuwa mshambuliaj ni miongoni mwa waliouawa. 

Watu wasiopungua 16 wamejeruhiwa na wamepelekwa katika hospitali mbaimbali kwa matibabu. 

Shambulizi hilo linajiri katika muda wa saa 24, baada ya kutokea mkasa mwengine kama huo ambapo watu 20 waliuawa na 26 kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki ndani ya duka moja kubwa eneo la El Paso, Texas. 

Polisi wamemkamata mwanaume anayeshukiwa kuhusika kwenye shambulizi la Texas mwenye umri miaka 21.

Msemaji wa polisi wa El Paso Robert Gomez ameeleza kuwa wengi wa wahanga katika kisa cha Texas walimiminiwa risasi katika duka la Walmart. 

Gomez ameongeza kuwa wakati wa tukio hilo kulikuwa na karibu wateja 3000 kwenye duka. 

Polisi wamesema huenda shambulizi hilo lilichochewa na chuki za ubaguzi wa rangi. 

Jumla ya watu 30 wameuawa kwenye mashambulizi hayo mawili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527