GARI LA MKUU WA MKOA WA MARA ADAM MALIMA LAPATA AJALI LIKIDAIWA KUENDESHWA NA MTOTO WA DEREVA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 5, 2019

GARI LA MKUU WA MKOA WA MARA ADAM MALIMA LAPATA AJALI LIKIDAIWA KUENDESHWA NA MTOTO WA DEREVA

  Malunde       Monday, August 5, 2019

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema gari la mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima limepata ajali jana Jumapili Agosti 4, 2019 likiwa linaendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wa dereva wa mkuu huyo wa Mkoa.

Ndaki amesema ajali hiyo imetokea  jana saa 3 asubuhi na kwamba gari hilo lenye namba za usajili STL 5961 lilikuwa likiendeshwa na mtu ambaye taarifa za awali zinaeleza kuwa ni kijana wa dereva wa Malima.

"Mtoto na Baba yake wote wamelazwa Hospitali, Mtoto ana majeraha baada ya kupata ajali na gari ya Mkuu wa Mkoa na huyu baba ambaye ni Dereva wa Mkuu wa Mkoa alianguka kwa Presha tukamkimbiza Hospitali, maana alipata mshtuko bada ya kufika eneo la tukio na kuiona ajali"-Amesema


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post