WAZIRI MKUU AAGIZA WAFUGAJI KUACHA TABIA YA KUCHORA CHORA NG'OMBEWaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza wafugaji wa ng’ombe mkoani Kagera kuacha mara moja vitendo vya kuchora chora ng'ombe kwa kuwawekea alama za manundu vidonda badala yake watumie pete ya sikioni ili kuongeza ubora na thamani utakaowavutia wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo Agosti 14,2019 katika uzinduzi wa Mwongozo wa wiki ya uwekezaji Kagera uliofanyika katika uwanja wa Gymkana uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera

Waziri mkuu amesema kuwa wafugaji walio wengi wamekuwa na utamaduni wa kuchora chora mifugo hao jambo linalosababisha kukosekana kwa soko la nje kwa wahitaji ambapo wahitaji hudai kuwa Ng’ombe hao hawana mvuto na ubora kwa kuonekana na vidonda ambavyo ni alama zisizofaa.

Kufuatia Agizo amewataka wafugaji kubadilika kwa kutumia lanchi za wilaya na kuacha kuzunguka zunguka na mifugo badala yake waiache mifugo hiyo ikue iwe katika ubora unaohitajika.

Hata hivyo ametoa kibali kwa wawekezaji kutoka nje kuwekeza mkoani Kagera kwa kujenga viwanda vya kuchakata Nyama Ngozi na kwato kwa kufuata utaratibu wa kiserikali usio na masharti magumu

Uzinduzi huo wa Mwongozo wa wiki ya uwekezaji Kagera umeudhuliwa na Magavana wa nchi ya Burundi, mabalozi kutoka Nchi za Kenya Uganda Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wajasiliamali mbali mbali toka ndani na nje ya nchi pamoja na , wakuu wa mikoa ya Tanzania, ambapo wiki hii ina lengo la kutangaza fulsa zilizopo Kagera na imeanza Agosti 12 mwaka huu itamalizika August 17 mwaka huu.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post