RC MNYETI AWATAKA WAKURUGENZI KUIGA HALMASHAURI YA KITETO

Na Beatrice Mosses - Malunde1 blog Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amewataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kwenda kuiga mfano kwa mkurugezi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto namna anavyotekeleza majukumu yake kikamilifu.


Mnyeti ameyasema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili na kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  na kuwapongeza kwa kupata hati safi.

Mnyeti amesema katika halmshauri na wilaya ambazo huwa hafikirii sana ni kwa namna gani atakwenda ni Kiteto kutokana na kuwa viongozi wake ni wasikivu, waelewa na wachapa kazi.

“Nizidi kuwapongeza sana endeeleni kushirikiana, kushikamana, kuheshimiana endeleeni kupendana hizi kazi za serikali usijitutumue kuwa wewe ni mkubwa kuliko kila mtu.

“Mkurugenzi huyu ni mchapa kazi sana na ninyi ni mashahidi kwa kazi anazofanya hapa ni kazi za mfano na mimi nimetuma sana wakurugenzi kuja kujifunza Kiteto mkurugenzi mwenzenu anafanya nini.

“Kuna mabweni hapa anajenga kwa mil. 150 ya kukaa watoto 180, kuna maeneo megine mabweni hayo hayo yaliyojengwa kwa mil. 150 yanajengwa kwa mil. 220 kuna mabweni hapa yanajengwa kwa mil. 75 ya kukaa vijana 80 mabweni hayo hayo ukienda maeneo mangine yanajengwa kwa mil. 150.

“Yeye anatumia mbinu gani na sio kwamba labda amejenga mafeki feki na wakaguzi wote waliokagua wanasema this is a proper kwa sababu kama ingekuwa ni mafeki tungejua kwamba aa huyu anatubabaisha ili atuonyeshe kwamba yeye anajua sana lakini majengo yanayojengwa yapo ndani ya kiwango makubwa na mazuri .

“Lakini ukichunguza kwa undani unagundua kwamba wale wengine wanakula hela, ni hela zinaliwa unakuta injinia amekaa na mkurugenzi au hata mkurugenzi hajui wataalamu wake wanamzunguka ka senti kanaondoka",alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post